Maono Yetu: Mazingira na Mali Asili Iliyosimamiwa Vyema kwa Manufaa ya Watu na Wanyama Pori.

Kuhusu Africa Nature

Africa Nature ni shirika lisilo la ki-Serikali lililo na afisi zake nchini Kenya lenye jukumu la kuc...

Read more...

Kazi Zetu

Kazi zetu zimepangwa kwa dhamira tatu. Dhamira hizi ni uhifadhi, mashirika ya kijamii na uchumi wa j...

Read more...

Washirika Wetu

Tunashirikiana na wafadhili, Serikali, mashirika yasiyo ya Serikali na jamii mashinani kukuza mbinu ...

Read more...

Changa kupitia Intaneti

<h4 id="ong">Changa kupitia Mtandao wa Intaneti</h4> Unaweza kuchanga kwa usalama kupitia PayPal ku...

Read more...
About Us Image

Africa Nature Organization ni nani?

Kuweko kwa uhitaji wa shirika la mashinani la kuunganisha jamii katika bara la Africa ili waweze kuchangia vilivyo kwa usimamizi endelevu wa mazingira na mali asili lilikuwa wazo lililobuniwa Arusha, Tanzania na wadau katika sekta ya mazingira na mali asili kutoka nchi mbali mbali Africa. Mazungumzo yaliendelea 20111 na hatimaye shirika la Africa Nature likabuniwa na kuandikishwa kama Shirika Lisilo la Kiserikali tarehe 2 Februari 2012, ambayo pia ilikuwa siku ya kimataifa ya kusherehekea maeneo lowevu duniani. Africa Nature linalenga kukuza mbinu na desturi endelevu za usimamizi wa mazingira na mali asili kwa ushirikiano wa karibu na jamii mashinani, mashirika ya kijamii, mashirika ya kibinafsi pamoja na Serikali.

Habari za Hivi Punde na Matukio

Sekta ya Mazingira na Mali Asili ilipata msukumo kwa kuzinduliwa kwa hazina ya miradi itakayo simamiwa na shirika la Act! Hazina hii kwa jina Changieni Rasili Mali (CRM), ni mpango wa miaka minne unaofadhiliwa na Serikali ya Sweden na Shirika la Serikali ya Uingereza la Misaada ya Kimataifa (UKaid). Changieni Rasili Mali ilizinduliwa rasmi tarehe […]

Kenya, kama nchi nyingine zinazoendelea, iko katika njia panda katika kukimu mahitaji ya kawi kwa kuendeleza uchumi na maendeleo. Uhaba wa kawi umeongezaka maradufu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya mara kwa mara ya bei za mafuta. Kupatikana kwa mafuta eneo la Turkana na gesi kidogo sehemu ya pwani ya Kenya […]

Afisi ya Makubaliano ya Ramsar kuhusu Maeneo Lowevu imetangaza katika tuvuti yake kuorodheshwa kwa eneo la Tana Delta kama Eneo Muhimu Lowevu la Kimataifa tarehe 12 Oktoba 2012. Sehemu ya Tana Delta ina ukubwa wa hekta 163,600 lipatikanalo 02°27’S 040°17’E. Eneao hili linajulikana kama sehemu muhimu ya ndege katika Pwani ya Kenya na sehemu ya […]