Hazina ya Kuboresha Usimamizi wa Mali Asili Yazinduliwa Nchini Kenya!

act3

Sekta ya Mazingira na Mali Asili ilipata msukumo kwa kuzinduliwa kwa hazina ya miradi itakayo simamiwa na shirika la Act! Hazina hii kwa jina Changieni Rasili Mali (CRM), ni mpango wa miaka minne unaofadhiliwa na Serikali ya Sweden na Shirika la Serikali ya Uingereza la Misaada ya Kimataifa (UKaid). Changieni Rasili Mali ilizinduliwa rasmi tarehe 21 Novemba 2012 katika hoteli ya Norfolk mjini Nairobi. Changieni Rasili Mali itawezesha wananchi na hasa wale waliotengwa kuhusika kikamilifu katika shughuli za usimamizi bora wa mali asili nchini Kenya.

Mgeni wa Heshima katika uzinduzi huu alikuwa Makamu wa Rais Mhe. Stephen Kalonzo Musyoka. Wageni wengine mashuhuri walioshuhudia uzinduzi huu walikuwa ni Bw. Anders J. Ronquist, Mkuu wa Ushirikiano Bora wa Maendeleo katika Ubalozi wa Sweden nchini Kenya, Bw. Alistair Fernie, kutoka Afisi ya UKaid Kenya, maafisa kutoka Wizara ya Mazingira na Mali Asili, pamoja na zaidi ya washikadau arubani wanaofadhiliwa na hazina hii.

Mhe. Stephen Kalonzo Musyoka katika hotuba yake, alikariri kuwa changamoto zinazokumba usimamizi wa mazingira na mali asili ni nyingi lakini zinaweza kabiliwa. Alipongeza Act! kwa kuanzisha hazina ya CRM mahusi kukabiliana na changamoto hizi. Alisisistiza kuwa CRM itachangia zaidi katika usimamizi endelevu wa mazingira na mali asili nchini Kenya. Aliongeza kusema kuwa CRM pamoja na mchango kutoka kwa miradi ya Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Mashirika ya Kibinafsi yatachangia pa kubwa katika kutimiza malengo ya mazingira ya Ruwaza ya 2030. Alishukuru sana Serikali ya Sweden na ya Uingereza kwa kufadhili CRM na kuwapa changamoto wafadhiliwa kushughulikia vilivyo maswala ya mazingira popote walipo, ikiwemo changamoto za mto Nairobi.
Wawakilishi wa Serikali ya Sweden pamoja na wa UKaid katika hotuba yao walisema walitiwa moyo sana na juhudi zinatofanywa na wafadhiliwa wa CRM na walitazamia kuwa juhudi zao zitachangia mabadiliko katika mashirika, chuma riziki na mazingira kwa jumla.
Mbali na hotuba, sherehe hii pia ilikuwa na nyimbo, maonyesho ya video ya Act! na hatimaye uzinduzi rasmi wa nembo ya CRM. Uzinduzi wa nembo ya CRM ulifanywa na Mgeni wa Heshima, Mhe. Stephen Kalonzo Musyoka.

Shirika la Africa Nature lilihudhuria sherehe hii kupitia Friends of Lake Ol Bolossat (FOLO). Africa Nature, kupitia kwa wafanyikazi wake wa kujitolea (Volunteers for Nature) walichangia pa kubwa katika kuhamasisha jamii kuandika barua za maombi ya ufadhili ya FOLO kwa Act! na CDTF (Community Development Trust Fund), maombi ambayo yalikubaliwa na kufadhiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *