Kazi Zetu

web-partners-c

Kazi zetu zimepangwa kwa dhamira tatu. Dhamira hizi ni uhifadhi, mashirika ya kijamii na uchumi wa jamii

Elimu Mazingira na Hamasisho la Jamii

Kampeni za kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu mazingira zimetambulika kubadisha tabia na mtazamo wa wadau kuhusu mazingira na mali asili. Kampeni za Shirika la Africa Nature zimelenga vijana na wazee kupitia mpango wa vijana (Young People4Nature), maonyesho, uadhimishaji wa siku za kimataifa za mazingira, kutembeleana, warsha za mafundisho

Uhifadhi wa Viumbe na Makao

Kutokana na tisho la kuangamia kwa viumbe na makao yao, iliyozidishwa makali na mabadiliko ya hali ya hewa, Shirika la Africa Nature imevutiwa mno na mipango ya kuhifadhi na kulinda viumbe na maeneo yao. Shughuli zinazozingatiwa zaidi ni upanzi wa miti na matumbawe baharini, kujenga vizuio vya maji, kutengeneza mikakati ya usimamizi was rasili mali na kusaidia jamii kulinda vimbe na maeneo yao.

Biashara Mazingira

Jamii tangu jadi wametegemea mali asili kujikimu kimaisha. Lakini, kutokana na upungufu wa mali asili kutokana na biashara, ongezeko la watu na mabadiliko ya hali ya hewa, jamii imejipata imenaswa katika mtego wa kuangamiza mali asili wanapojitafutia riziki za kila siku. Kuondoa janga hili, Shirika la Africa Nature linafanya kazi kwa karibu na jamii mashinani kuwawezesha kubuni biashara mazingira na kuwaunganisha na masoko.

Utafiti na Ubunifu kwa Mazingira

Habari muhimu za kuwezesha maamuzi muafaka kuhusu mali asili zimekuwa kikwazo katika usimamizi endelevu wa mazingira na mali asili. Changamoto hizi zimekumba jamii mashinani na hata mashirika ya kijamii na ya ki-Serikali yanayosaidia jamii kusimamia rasili mali hizi. Kuthibiti changamoto hii, Shirika la Africa Nature linatafiti na kubuni mbinu muafaka za usimamizi na matumizi bora ya mali asili. Utafiti msingi wa miradi, utathmini wa athari ya miradi kwa mazingira, uandikishaji wa nyaraka za elimu mazingira ya kiatamaduni, matumizi bunifu ya teknolojia kwa mazingira ni baadhi ya shughuli tunazofanya.

Taarifa za Uhifadhi

Mawasiliano ya taarifa za uhifadhi kwa washika dau ni muhimu katika kuwahusisha katika juhudi za uhifadhi. Mawasiliano na taarifa zinahakikisha wadau wana moyo wa uhifadhi kupitia: –

  • Kijarida
  • Filamu za uhifadhi
  • Utoaji wa taarifa nyinginezo za elimu mazingira