Kuhusu Africa Nature

community-iniitiatives-on-clean-energy-crop

Africa Nature ni shirika lisilo la ki-Serikali lililo na afisi zake nchini Kenya lenye jukumu la kuchangia usimamizi bora wa mazingira na mali asili kwa manufaa ya binadamu na wanyama pori.

Africa Nature Organization ni nani?

Kuweko kwa uhitaji wa shirika la mashinani la kuunganisha jamii katika bara la Africa ili waweze kuchangia vilivyo kwa usimamizi endelevu wa mazingira na mali asili lilikuwa wazo lililobuniwa Arusha, Tanzania na wadau katika sekta ya mazingira na mali asili kutoka nchi mbali mbali Africa. Mazungumzo yaliendelea 20111 na hatimaye shirika la Africa Nature likabuniwa na kuandikishwa kama Shirika Lisilo la Kiserikali tarehe 2 Februari 2012, ambayo pia ilikuwa siku ya kimataifa ya kusherehekea maeneo lowevu duniani. Africa Nature linalenga kukuza mbinu na desturi endelevu za usimamizi wa mazingira na mali asili kwa ushirikiano wa karibu na jamii mashinani, mashirika ya kijamii, mashirika ya kibinafsi pamoja na Serikali.

Maono Yetu

Mazingira na mali asili iliyosimamiwa vyema kwa manufaa ya watu na wanyama pori.

Wajibu Wetu

Kuboresha usimamizi endelevu wa mazingira na mali asili kwa kuwawezesha jamii mashinani, kusaidia kutengeneza sera, sheria na mbinu muafaka za usimamizi bora wa mali asili, kukuza mbinu na desturi bora za matumizi ya mali asili.

Utawala

ANO ina bodi ya utawala ya wanachama watano wenye uzoefu na ustadi katika Nyanja mbalimbali za mazingira, simamizi wa mali asili, ujenzi wa uwezo wa wadau, utetezi wa sera na utafiti

Maadili Msingi

Shirika la Africa Nature linaongozwa na maadili yafuatayo katika kutekeleza shughuli zake: –

  1. Usawa na Haki: AWatu wote wana haki ya kupata manufaa ya mazingira na mali asili. Kwa kuzingatia haya, ukuzaji na usambazaji wa manufaa haya lazima yazingatie ubora na manufaa ya mazingira na mali asili, na kutambua usawa na haki za vizazi vilivyoko na vijavyo.
  2. Matumizi Endelevu: Tunaamini kuwa matumizi endelevu ya mazingira na mali asili itadumisha manufaa kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.
  3. Ushirikiano: Tunatambua kuwa kazi ya kujenga miundo thabiti ya usimamizi wa mazingira na mali asili ni kubwa. Kwa kutimiza wajibu wetu na kuchangia kikamilifu, tutafanya kazi kwa karibu na jamii mashinani, mashirika ya jamii, mashirika na kampuni za kibinafsi na Serikali.
  4. Taaluma: Tumejitolea kufuata maono yetu na kutimiza wajibu wetu. Tutatimiza wajibu wetu kwa uangalifu na bidii kwa kuzingatia maadili yanayotambulika kitaifa na hat kimataifa.
  5. Kubadilika: Tunafanya kazi katika mazingira ambayo yanabadilika mara kwa mara, na kwa hivyo tutabadilisha mbinu, mikakati na vifaa kulingana na mabadiliko ya mazingira ya kazi