Majukwaa Yetu

Shirika la Africa Nature limeunda majukwa ili kuongeza uhusiano na juhudi za ushirikiano na wadau wake. Majukwaa haya ni People4Nature Global, Mtandao wa Kimataifa wa Wataalam wa Maji (iNoWPractice), Anzisho la Jamii la Kuongeza Ugavi wa Manufaa ya Rasili Mali za Ki-biolojia Africa (Africa.II.ABS).

Mtandao wa People4Nature Global

People4Nature Global ni mtandao usio na mipaka kwa watu binafsi wapendao mazingira na vile mazingira yanavyosaidia kukuza na kuboresha maisha ya bionadamu. People4Nature Global inawapa fursa kwa wanachama wao ya kubadilishana habari, elimu na uzoefu kutokana na matumizi ya mazingira na mali asili. Jukwa hili linanuia kuwawezesha watu binafsi na jamii kutumia vyema mazingira na mali asili kwa kuelimisha, kuhamasisha na kuanzisha na kuendeleza bishara mazingira.
Jukwaa hili pia ni kifaa muhimu cha kukusanya na kutafuta rasili mali muhimu za kuwezesha usimamizi endelevu na matumizi bora ya mali asili nyumbani, vijijini, nchini, barani na hata katika ngazi ya kimataifa.

Kujiunga na People4nature, fuata KIUNGANISHI hiki.

iNoW Practice

Mtandao wa Kimataifa wa Wataalam wa Maji (iNoWPractice) unalenga kukuza usimamizi bora wa rasili mali ya maji. Unaleta pamoja wataalam wa maji kujadiliana na kupanga mikakati ya usimamizi endelevu wa maji duniani.

Africa.II.ABS

Anzisho la Jamii la Kuongeza Ugavi wa Manufaa ya Rasili Mali za Ki-biolojia Africa (Africa.II.ABS) ni jukwa la jamii mashinani na hasa jamii zilizolinda tamaduni na mazingira yao ili kutetea na kuongeza ugavi wa manufaa yanaypotoka na elimu tamaduni na rasili mali za ki-biolojia