{"id":1430,"date":"2023-08-09T20:03:15","date_gmt":"2023-08-09T17:03:15","guid":{"rendered":"https:\/\/africanature.or.ke\/?p=1430"},"modified":"2023-08-10T15:38:20","modified_gmt":"2023-08-10T12:38:20","slug":"madunguni-forest","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/madunguni-forest\/","title":{"rendered":"MSITU WA MADUNGUNI - Msitu Asili Wa Pwani Ya Kenya Unaoangamia Polepole\u00a0"},"content":{"rendered":"<p><em>Waandishi wa Makala: Bw. Raphael Ngumbao, Mwenyekiti, Friends of Madunguni Forest, na mwanachama, Watu Mazingira Ulimwenguni.\u00a0<\/em><\/p>\n<hr \/>\n<p>Msitu wa Madunguni ni msitu wa serikali wenye eneo la heka 951.85. Msitu huu ni moja wa misitu asili ya sehemu kame za pwani. Unapatikana kaskazini mashariki mwa msitu mashuhuri wa Arabuko Sokoke. Barabara ya Malindi-Sala Gate inagawanya misitu hii\nmiwili.Msitu wa Madunguni, ni hifadhi ya wanyama na miti asili inayopatika tu katika eneo hili la Madunguni-Arabuko Sokoke. Ni masilikitiko kuwa msitu wa Madunguni umeendelea kuzorota kutokana na uvamizi wa maskwota, watengeza makaa, wavuna mbao na wanao tafuta kuni za kuuza.<\/p>\n<p>Ina kadiriwa kuwa asili mia 75 ya msitu umepotea tangu miaka ya 1980 kwa sababu ya uvamizi huu. Madhara yake yamekuwa mmomonyoko wa udongo unao athiri mashamba na makazi sehemu za chini ya Madunguni. Mmomonyoko huu umeleta maporomoko makubwa sehemu kadhaa za msitu.<\/p>\n<p>Msitu wa Madunguni ulipata jina lake kutoka kwa kijiji cha Madunguni, kinacho julikana kwa mashamba yaliyo na rotuba na sehemu muhimu ya kuzalisha chakula kwa Kaunti ya Kilifi. Dungu, ambapo wingi wake ni madungu, ni nyumba iliyo inuliwa kwa miti ili kukinga wakulima\ndhidi ya uvamizi wa simba na wanyama wengine wa pori.<\/p>\n<p>Msitu wa Madunguni awali ulikuwa chini ya usimamizi wa Serikali za Wilaya. Na kwa wenyeji wa Madunguni waliuhifadhi kwa sababu ya kupata kuni kwa vile hawakuwa na ruhusa ya kuingia katika msitu wa Serikali wa Arabuko Sokoke. Lakini muhimu zaidi ni kwamba, wenyeji walitumia msitu huu kutabiri mvua na hali ya hewa. Na kwa hivyo, palikuwa sehemu takatifu kwa wenyeji.<\/p>\n<p>Lakini mambo yalianza kubadilika kuanzia 1969. Wakaazi wa eneo la Maili 10 ya pwani, ikijulikana wakati huo kama Mikaoni, walianza kuvamia msitu wakitafuta kuni, mbao, kulima na hata kutengeneza makaaa. Sehemu ya Mikaoni ilijumuisha vijiji vya Kakuyuni, Mere na Mida.<\/p>\n<p>Mnamo 1971, jamii ya Madunguni pamoja na Afisa wa Misitu, Bw. Tinga, waliarifu Serikali\nya Mkoa kuhusu uharibifu huu. Machifu Awadh na Athmani Ndurya, wa sehemu ya Mikaoni, walipewa jukumu la kusitisha uharibifu huu kutoka kwa wakaazi wanaotoka sehemu zao.\n\nKutokana na ushirikiano wa Afisa wa Misitu na jamii ya Madunguni, kijiji cha Madunguni waliweza kuunda Kamati ya Mazingira ya Madunguni.<\/p>\n<p>Mwaka huu pia Idara ya Misitu ilinuia kujenga kituo kidogo cha utafiti eneo la Arabuko Sokoke ndani ya Msitu wa Madunguni. Lakini wenyeji wa Madunguni wakiongozwa na mwenyekiti wa\nKamati ya Mazingira ya Madunguni, Bw. Ngumbao Mwanzili, hawa kukubaliana na wazo hilo. Wangekubali, pengine msitu wa Madunguni ungebadilishwa kuwa wa Serikali.<\/p>\n<p>Kufikia 1980, uharibifu wa msitu ulikuwa umekithiri. Bw. Ngumbao Mwanzili alipata kuungwa mkono na Bw. Kaingu Bindurya na Abdalla Ndema, wakereketwa waliosaidia kuhamasisha jamii kuhusu uharibifu wa msitu. Kwa juhudi zao, wavamizi walifurushwa na Serikali ya Mkoa na kujipatia makao karibu na msitu. Kufikia 1987, wavamizi walirudi tena kufanya makao na kuendelea kulima ndani ya msitu.<\/p>\n<p>Idadi ya wavamizi iliendelea kuongezeka hadi 500 mwaka wa 1996. Wanasiasa pia wakaingilia\nswala la msitu wa Madunguni na kuwapa moyo wavamizi kuendelea kulima. Hali ilibadilika\nwakati wavamizi wa zamani na wapya walipoanza kuteta wenyewe kwa wenyewe. Wengine\nwalipoteza maisha yao katika vita hivyo.<\/p>\n<p>Serikali ya Mkoa ilishindwa kukabiliana na mwingilio wa wanasiasa katika kutatua mzozo\nwa msitu. Hatimaye, iliwabidi kuwafurusha wavamizi badala ya kuwapeleka kortini ambako\nwanasiasa walisaidia kurushwa kwa kesi zao.<\/p>\n<p>Vijana wa Madunguni pia hawa kuachwa nyuma katika harakati za kuokoa msitu wao. Mnamo 2001, vijana waliunda na kusajili Friends of Madunguni Forest, kama njia moja ya kusaidia juhudi za Kamati ya Mazingira ya Madunguni. Mwaka 2004, pamoja na wadau wengine waliweza kumshawishi Mbunge wa Malindi, Bw. Abubakar Badawy kupeleka mswada bunge\nwa kubadilisha msitu huo kuwa wa Serikali. Na ombi hilo likapitishwa.<\/p>\n<p>Wavamizi nao hawa kuachwa nyuma. Waliweza kupeleka kesi kortini kupinga kuorodheshwa\nkwa msitu kuwa wa Serikali. Korti iliamuru wavamizi wabaki bila kufanya shughuli zozote ndani ya msitu hadi kesi itakapo amuliwa.<\/p>\n<p>Kesi bado haija amuliwa. Kwa muda huu, msitu umeendelea kuharibiwa bila kujali amri ya Korti.<\/p>\n<p>Ukulima, utengenezaji makaa, na ujenzi wa shule, makanisa na msikiti zimeendelea ndani ya msitu. Idadi ya wavamizi pia imezidi kuongezeka hadi takriban watu 2000, na wana amini kuwa siku moja Serikali itachoka na kuwaachia msitu.<\/p>\n<p>Kulingana na shughuli zote zinazo endelea ndani ya msitu, inakadiriwa kuwa msitu wa Madunguni utaangamia chini ya miaka 5. Athari kubwa Zaidi haitakuwa tu kwa msitu, bali pia kwa wakaazi wa Madunguni ambao mashamba yao yamepoteza rotuba kutokana na limbikizo la udongo usio rotuba kutoka msituni.<\/p>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Written by: Mr. Raphael Ngumbao, Chairman, Friends of Madunguni Forest, Mr. Charles Thoya, Chairman, Jilore Community Forest Association, and Mr. Weston Mure, resident and member of People4Nature Global.\u00a0 The Madunguni [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":1,"featured_media":1431,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_price":"","_stock":"","_tribe_ticket_header":"","_tribe_default_ticket_provider":"","_tribe_ticket_capacity":"0","_ticket_start_date":"","_ticket_end_date":"","_tribe_ticket_show_description":"","_tribe_ticket_show_not_going":false,"_tribe_ticket_use_global_stock":"","_tribe_ticket_global_stock_level":"","_global_stock_mode":"","_global_stock_cap":"","_tribe_rsvp_for_event":"","_tribe_ticket_going_count":"","_tribe_ticket_not_going_count":"","_tribe_tickets_list":[],"_tribe_ticket_has_attendee_info_fields":false,"_themeisle_gutenberg_block_has_review":false,"footnotes":""},"categories":[37],"tags":[],"class_list":["post-1430","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-blog"],"yoast_head":"<!-- This site is optimized with the Yoast SEO Premium plugin v20.13 (Yoast SEO v21.5) - https:\/\/yoast.com\/wordpress\/plugins\/seo\/ -->\n<title>MADUNGUNI FOREST - A Remnant Indigenous Coastal Forest Dying a Slow, Painful Death.\u00a0 - Africa Nature Organization<\/title>\n<meta name=\"robots\" content=\"index, follow, max-snippet:-1, max-image-preview:large, max-video-preview:-1\" \/>\n<link rel=\"canonical\" href=\"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/madunguni-forest\/\" \/>\n<meta property=\"og:locale\" content=\"en_US\" \/>\n<meta property=\"og:type\" content=\"article\" \/>\n<meta property=\"og:title\" content=\"MADUNGUNI FOREST - A Remnant Indigenous Coastal Forest Dying a Slow, Painful Death.\u00a0\" \/>\n<meta property=\"og:description\" content=\"Written by: Mr. Raphael Ngumbao, Chairman, Friends of Madunguni Forest, Mr. Charles Thoya, Chairman, Jilore Community Forest Association, and Mr. Weston Mure, resident and member of People4Nature Global.\u00a0 The Madunguni [&hellip;]\" \/>\n<meta property=\"og:url\" content=\"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/madunguni-forest\/\" \/>\n<meta property=\"og:site_name\" content=\"Africa Nature Organization\" \/>\n<meta property=\"article:publisher\" content=\"https:\/\/www.facebook.com\/AfricaNatureOrg\/\" \/>\n<meta property=\"article:published_time\" content=\"2023-08-09T17:03:15+00:00\" \/>\n<meta property=\"article:modified_time\" content=\"2023-08-10T12:38:20+00:00\" \/>\n<meta property=\"og:image\" content=\"https:\/\/africanature.or.ke\/wp-content\/uploads\/2023\/08\/Article-1-madunguni-scaled.jpg\" \/>\n\t<meta property=\"og:image:width\" content=\"2560\" \/>\n\t<meta property=\"og:image:height\" content=\"1707\" \/>\n\t<meta property=\"og:image:type\" content=\"image\/jpeg\" \/>\n<meta name=\"author\" content=\"Africa Nature Organization\" \/>\n<meta name=\"twitter:card\" content=\"summary_large_image\" \/>\n<meta name=\"twitter:creator\" content=\"@africanatureorg\" \/>\n<meta name=\"twitter:site\" content=\"@africanatureorg\" \/>\n<meta name=\"twitter:label1\" content=\"Written by\" \/>\n\t<meta name=\"twitter:data1\" content=\"Africa Nature Organization\" \/>\n\t<meta name=\"twitter:label2\" content=\"Est. reading time\" \/>\n\t<meta name=\"twitter:data2\" content=\"dakika 4\" \/>\n<script type=\"application\/ld+json\" class=\"yoast-schema-graph\">{\"@context\":\"https:\/\/schema.org\",\"@graph\":[{\"@type\":\"Article\",\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/#article\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/\"},\"author\":{\"name\":\"Africa Nature Organization\",\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/#\/schema\/person\/f2ae82b645270a7a54d96b885a686efb\"},\"headline\":\"MADUNGUNI FOREST &#8211; A Remnant Indigenous Coastal Forest Dying a Slow, Painful Death.\u00a0\",\"datePublished\":\"2023-08-09T17:03:15+00:00\",\"dateModified\":\"2023-08-10T12:38:20+00:00\",\"mainEntityOfPage\":{\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/\"},\"wordCount\":843,\"commentCount\":0,\"publisher\":{\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/#organization\"},\"articleSection\":[\"Blog\"],\"inLanguage\":\"sw\",\"potentialAction\":[{\"@type\":\"CommentAction\",\"name\":\"Comment\",\"target\":[\"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/#respond\"]}]},{\"@type\":\"WebPage\",\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/\",\"url\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/\",\"name\":\"MADUNGUNI FOREST - A Remnant Indigenous Coastal Forest Dying a Slow, Painful Death.\u00a0 - Africa Nature Organization\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/#website\"},\"datePublished\":\"2023-08-09T17:03:15+00:00\",\"dateModified\":\"2023-08-10T12:38:20+00:00\",\"breadcrumb\":{\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/#breadcrumb\"},\"inLanguage\":\"sw\",\"potentialAction\":[{\"@type\":\"ReadAction\",\"target\":[\"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/\"]}]},{\"@type\":\"BreadcrumbList\",\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/#breadcrumb\",\"itemListElement\":[{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":1,\"name\":\"Home\",\"item\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":2,\"name\":\"MADUNGUNI FOREST &#8211; A Remnant Indigenous Coastal Forest Dying a Slow, Painful Death.\u00a0\"}]},{\"@type\":\"WebSite\",\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/#website\",\"url\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/\",\"name\":\"Africa Nature Organization\",\"description\":\"People4Nature\",\"publisher\":{\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/#organization\"},\"potentialAction\":[{\"@type\":\"SearchAction\",\"target\":{\"@type\":\"EntryPoint\",\"urlTemplate\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/?s={search_term_string}\"},\"query-input\":\"required name=search_term_string\"}],\"inLanguage\":\"sw\"},{\"@type\":\"Organization\",\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/#organization\",\"name\":\"Africa Nature Organization\",\"alternateName\":\"Africa Nature Organization\",\"url\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/\",\"logo\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw\",\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/#\/schema\/logo\/image\/\",\"url\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/cropped-logo.png\",\"contentUrl\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/cropped-logo.png\",\"width\":207,\"height\":50,\"caption\":\"Africa Nature Organization\"},\"image\":{\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/#\/schema\/logo\/image\/\"},\"sameAs\":[\"https:\/\/www.facebook.com\/AfricaNatureOrg\/\",\"https:\/\/twitter.com\/africanatureorg\"]},{\"@type\":\"Person\",\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/#\/schema\/person\/f2ae82b645270a7a54d96b885a686efb\",\"name\":\"Africa Nature Organization\",\"image\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw\",\"@id\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/#\/schema\/person\/image\/\",\"url\":\"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/65d22afb4dcab04b77cb092cf91c70cdc327e00c0f43fbc8663ae731678462c9?s=96&d=mm&r=g\",\"contentUrl\":\"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/65d22afb4dcab04b77cb092cf91c70cdc327e00c0f43fbc8663ae731678462c9?s=96&d=mm&r=g\",\"caption\":\"Africa Nature Organization\"},\"sameAs\":[\"https:\/\/africanature.or.ke\/demo\"],\"url\":\"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/author\/admin_an\/\"}]}<\/script>\n<!-- \/ Yoast SEO Premium plugin. -->","yoast_head_json":{"title":"MADUNGUNI FOREST - A Remnant Indigenous Coastal Forest Dying a Slow, Painful Death.\u00a0 - Africa Nature Organization","robots":{"index":"index","follow":"follow","max-snippet":"max-snippet:-1","max-image-preview":"max-image-preview:large","max-video-preview":"max-video-preview:-1"},"canonical":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/madunguni-forest\/","og_locale":"en_US","og_type":"article","og_title":"MADUNGUNI FOREST - A Remnant Indigenous Coastal Forest Dying a Slow, Painful Death.\u00a0","og_description":"Written by: Mr. Raphael Ngumbao, Chairman, Friends of Madunguni Forest, Mr. Charles Thoya, Chairman, Jilore Community Forest Association, and Mr. Weston Mure, resident and member of People4Nature Global.\u00a0 The Madunguni [&hellip;]","og_url":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/madunguni-forest\/","og_site_name":"Africa Nature Organization","article_publisher":"https:\/\/www.facebook.com\/AfricaNatureOrg\/","article_published_time":"2023-08-09T17:03:15+00:00","article_modified_time":"2023-08-10T12:38:20+00:00","og_image":[{"width":2560,"height":1707,"url":"https:\/\/africanature.or.ke\/wp-content\/uploads\/2023\/08\/Article-1-madunguni-scaled.jpg","type":"image\/jpeg"}],"author":"Africa Nature Organization","twitter_card":"summary_large_image","twitter_creator":"@africanatureorg","twitter_site":"@africanatureorg","twitter_misc":{"Written by":"Africa Nature Organization","Est. reading time":"dakika 4"},"schema":{"@context":"https:\/\/schema.org","@graph":[{"@type":"Article","@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/#article","isPartOf":{"@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/"},"author":{"name":"Africa Nature Organization","@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/#\/schema\/person\/f2ae82b645270a7a54d96b885a686efb"},"headline":"MADUNGUNI FOREST &#8211; A Remnant Indigenous Coastal Forest Dying a Slow, Painful Death.\u00a0","datePublished":"2023-08-09T17:03:15+00:00","dateModified":"2023-08-10T12:38:20+00:00","mainEntityOfPage":{"@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/"},"wordCount":843,"commentCount":0,"publisher":{"@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/#organization"},"articleSection":["Blog"],"inLanguage":"sw","potentialAction":[{"@type":"CommentAction","name":"Comment","target":["https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/#respond"]}]},{"@type":"WebPage","@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/","url":"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/","name":"MADUNGUNI FOREST - A Remnant Indigenous Coastal Forest Dying a Slow, Painful Death.\u00a0 - Africa Nature Organization","isPartOf":{"@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/#website"},"datePublished":"2023-08-09T17:03:15+00:00","dateModified":"2023-08-10T12:38:20+00:00","breadcrumb":{"@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/#breadcrumb"},"inLanguage":"sw","potentialAction":[{"@type":"ReadAction","target":["https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/"]}]},{"@type":"BreadcrumbList","@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/madunguni-forest\/#breadcrumb","itemListElement":[{"@type":"ListItem","position":1,"name":"Home","item":"https:\/\/africanature.or.ke\/"},{"@type":"ListItem","position":2,"name":"MADUNGUNI FOREST &#8211; A Remnant Indigenous Coastal Forest Dying a Slow, Painful Death.\u00a0"}]},{"@type":"WebSite","@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/#website","url":"https:\/\/africanature.or.ke\/","name":"Africa Nature Organization","description":"People4Nature","publisher":{"@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/#organization"},"potentialAction":[{"@type":"SearchAction","target":{"@type":"EntryPoint","urlTemplate":"https:\/\/africanature.or.ke\/?s={search_term_string}"},"query-input":"required name=search_term_string"}],"inLanguage":"sw"},{"@type":"Organization","@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/#organization","name":"Africa Nature Organization","alternateName":"Africa Nature Organization","url":"https:\/\/africanature.or.ke\/","logo":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw","@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/#\/schema\/logo\/image\/","url":"https:\/\/africanature.or.ke\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/cropped-logo.png","contentUrl":"https:\/\/africanature.or.ke\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/cropped-logo.png","width":207,"height":50,"caption":"Africa Nature Organization"},"image":{"@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/#\/schema\/logo\/image\/"},"sameAs":["https:\/\/www.facebook.com\/AfricaNatureOrg\/","https:\/\/twitter.com\/africanatureorg"]},{"@type":"Person","@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/#\/schema\/person\/f2ae82b645270a7a54d96b885a686efb","name":"Africa Nature Organization","image":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw","@id":"https:\/\/africanature.or.ke\/#\/schema\/person\/image\/","url":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/65d22afb4dcab04b77cb092cf91c70cdc327e00c0f43fbc8663ae731678462c9?s=96&d=mm&r=g","contentUrl":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/65d22afb4dcab04b77cb092cf91c70cdc327e00c0f43fbc8663ae731678462c9?s=96&d=mm&r=g","caption":"Africa Nature Organization"},"sameAs":["https:\/\/africanature.or.ke\/demo"],"url":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/author\/admin_an\/"}]}},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1430","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1430"}],"version-history":[{"count":9,"href":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1430\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":1442,"href":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1430\/revisions\/1442"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media\/1431"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1430"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1430"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/africanature.or.ke\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1430"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}