KUHUSU AFRICA NATURE ORGANIZATION
Sisi ni nani
Haja ya kuwa na shirika la kuhamasisha jamii mashinani ili kuchangia kikamilifu katika usimamizi undelevu wa mali asili kote barani Afrika ni wazo lililo chipuza katika mjadala wa wanamazingira walio kongamana 2010 mjini Arusha, Tanzania.
Lengo letu limekuwa kukuza mbinu bora za usimamizi wa mazingira na maliasili miongoni mwa jamii mashinani, kufanya kazi kwa karibu na mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi na Serikali.