
Kupata habari muhimu za kuwezesha maamuzi mwafaka imekuwa kikwazo katika usimamizi endelevu wa mazingira na mali asili. Changamoto hizi zimekumba jamii mashinani na hata mashirika ya kijamii na ya ki-Serikali yanayosaidia jamii kusimamia rasili mali hizi. Kuthibiti changamoto hii, Shirika la Africa Nature Organization linatafiti na kubuni mbinu mwafaka za usimamizi na matumizi bora ya mali asili. Utafiti msingi wa miradi, utathmini wa athari ya miradi kwa mazingira, uandikishaji wa nyaraka za elimu mazingira ya kiatamaduni, matumizi bunifu ya teknolojia kwa mazingira ni baadhi ya shughuli tunazofanya.