0
Your Cart
No products in the cart.

Tunachofanya

Elimu ya Uhifadhi na Hamasisho

Kampeni za elimu ya uhifadhi na hamasisho za Shirika la Afrika Nature Organization zinalenga vijana na wazee kupitia kampeni kama vile Mipango ya Jukwaa la Vijana, maonyesho ya mbinu mwafaka za kulinda na kusimamia mazingira, siku muhimu za kimazingira, ziara za mafunzo, warsha na semina ni baadhi ya shughuli katika kitengo hiki.

Web-Partners-c-1
Conservation-of-Species

Uhifadhi wa Spishi na Makazi (Hifadhi)

Upanzi wa miti katika nchi kavu, upanzi wa matumbawe katika mifumo ikolojia ya bahari, ujenzi wa kuta, utengezaji wa mipango ya usimamizi, usaidizi kwa walinzi wa jamii wanaolinda na kufuatizia spishi na makazi, ni baadhi ya shughuli zinazo tekelezwa ili kupunguza athari ya kuangamia kwa spishi na makazi yake.

Mipango ya Uhifadhi inayoongozwa na Biashara (ECO).

Jamii kwa miaka mingi zimetegemea maliasili kwa chumo riziki zao. Hata hivyo, kutokana na kupungua kwa maliasili kwa sababu ya uvunaji kwa madhumuni ya biashara, ongezeko la watu na mabadiliko ya tabianchi, jamii zimenaswa katika gurudumo la kuharibu mazingira na maliasili ili kujikimu.

Enterprise-Led-Conservation

Utafiti na Ubunifu kwa Uhifadhi (RI-Conserve)

Taarifa muhimu za kusaidia kufanya maamuzi muhimu kuhusu maliasili zimekuwa kikwazo kwa usimamizi endelevu wa mazingira na maliasili. Hali hii limekuwa kero kwa jamii na mashirika mashinani, ikiwemo Serikali, walio mstari wa mbele kuwawezesha wadau kusimamia mazingira na maliasili kwa njia endelevu. Ili kuziba pengo hili, Shirika la Africa Nature Organization hufanya utafiti na kuunda njia bunifu za kukabiliana na changamoto za kimazingira zinazokabili jamii, mashirika ya kijamii, mashirika ya kibinafsi na serikali. Tafiti za kimsingi, tathmini za athari za kimazingira, uwekaji kumbukumbu za elimu tamaduni kuhusu rasilimali za kibiolojia, na teknolojia bunifu ya simu za rununu kwa ajili ya uhifadhi ni baadhi ya shughuli zinazo tekelezwa katika kitengo hiki.

swSwahili