Kampeni za kudumu za elimu ya uhifadhi na hamasisho zimetambuliwa kwa uwezo wake wa kubadilisha tabia na mitazamo ya washika dau kuhusu mazingira na maliasili.
Kampeni za elimu ya uhifadhi na hamasisho za Shirika la Afrika Nature Organization zinalenga vijana na wazee kupitia kampeni kama vile Mipango ya Jukwaa la Vijana, maonyesho ya mbinu mwafaka za kulinda na kusimamia mazingira, siku muhimu za kimazingira, ziara za mafunzo, warsha na semina ni baadhi ya shughuli katika kitengo hiki.