Watu Mazingira
Mashujaa wa Uhifadhi
WatuMazingira
WatuMazingira Ulimwenguni ni jukwaa la ushirikiano wa watu wanaopenda mazingira, kuyalinda, kuyahifadhi na kuendeleza matumizi endelevu kwa manufaa ya watu na mazingira kote ulimwenguni.
Mtandao wa WatuMazingira Ulimwenguni una maono ya ulimwengu ambao Watu wanaishi kwa kuyajali Mazingira. Hili, Watu Mazingira wanatarajia kuafikiwa kwa kuhamasisha jamii na kujenga desturi ya matumizi endelevu ya mazingira na maliasili.
Mtandao wa WatuMazingira Ulimwenguni umewapa wanachama wake jukwaa la kupashana habari, elimu, na uzoefu waliopata wanapotumia mazingira na maliasili. Mtandao huu unalenga kuwezesha watu binafsi na jamii kutumia mazingira na maliasili kwa njia endelevu kupitia elimu ya uhifadhi, hamasa, biashara endelevu za mazingira na desturi nyinginezo endelevu.

Shughuli za WatuMazingira
Shughuli za WatuMazingira zinaratibiwa na Ofisi ya Katibu kwa ushirikiano na Kamati Kuu ya WatuMazingira. Kuna majukwaa 8 ya ushirikiano kulingana na mandhari za kimazingira, kama ifuatvyo - Jukwaa la Maji (iNoWpracticeWater), Jukwaa la Biashara inayo Boresha Mazingira (ECO-P4N), Jukwaa la Jamii Asili (Indigenous P4N), Jukwaa la Wanyama Pori na Misitu (P4N-Wild), Jukwaa la Kilimo Hifadhi na Uvuvi (P4N-CAF), Jukwaa la Elimu ya Uhifadhi na Hamasisho (P4N-EnEA), Jukwaa la Vijana (YP4N) na Jukwaa la Wanawake (NoW Conservation).
Kujiandikisha na Mtandao wa WatuMazingira kuko wazi kwa kwa mtu yeyote aliye tayari kufuata malengo, mipango na tabia za WatuMazingira Ulimwenguni. Uanachama pia uko wazi kwa vijana chini ya miaka 18.

Faida za uanachama
Baadhi ya faida za uanachama ni pamoja na: -
1. Fursa ya kujihusisha na kutangamana na wasimamizi wa mazingira na maliasili, wapenda mazingira na wakaazi kote Ulimwenguni,
2. Jukwaa la kukuza mchango wako katika kuhamasisha umma kuhusu hali mazingira yetu na masuala ya uhifadhi,
3. Kushiriki katika shughuli za uhifadhi na mafunzo zilizoandaliwa na WatuMazingira,
4. Usaidizi wa kiufundi katika kutekeleza shughuli za uhifadhi,
5. Usaidizi wa kuanzisha na kukuza biashara endelevu za kimazingira, na fursa ya kufikia soko kubwa zaidi,
6. Kushiriki katika hafla zikiwemo Tuzo za Mwaka za WatuMazingira Ulimwenguni,
7. Kupokea jarida letu la kila robo mwaka la Watu Mazingira.

Kamati Kuu ya Watu Mazingira
Wanachama wa Watu Mazingira
Jazzy Rasolojaona
P4N 413, Antananarivo, Madagascar
Karim Unusa
P4N 429, Younde, Cameroon
Soledad Castro
P4N 320, San Jose, Costa Rica
Stephanie Jones
P4N-306, Virginia, USA
Dr. Muktarun Islam
P4N-404, Sylhet City, Bangladesh
Jiunge na WatuMazingira SASA!
Uanachama wetu uko wazi kwa mtu yeyote kote ulimwenguni. Hii inatuwezesha kuwa na matokeo mapana na bora katika juhudi zetu za kuhifadhi mazingira. Kuwa mwanachama wa WatuMazingira ni rahisi sana. Bonyeza kitufe kilicho hapa chini, kamilisha taratibu za kulipa na ulipe. Tutawasiliana nawe baada ya muda mfupi iweze kanavyo kukujulisha nambari yako ya uanachama na kukushirikisha katika mipango yetu mbalimbali. Karibu kwenye nyumbani!