Taarifa muhimu za kusaidia kufanya maamuzi muhimu kuhusu maliasili zimekuwa kikwazo kwa usimamizi endelevu wa mazingira na maliasili. Hali hii limekuwa kero kwa jamii na mashirika mashinani, ikiwemo Serikali, walio mstari wa mbele kuwawezesha wadau kusimamia mazingira na maliasili kwa njia endelevu. Ili kuziba pengo hili, Shirika la Africa Nature Organization hufanya utafiti na kuunda njia bunifu za kukabiliana na changamoto za kimazingira zinazokabili jamii, mashirika ya kijamii, mashirika ya kibinafsi na serikali. Tafiti za kimsingi, tathmini za athari za kimazingira, uwekaji kumbukumbu za elimu tamaduni kuhusu rasilimali za kibiolojia, na teknolojia bunifu ya simu za rununu kwa ajili ya uhifadhi ni baadhi ya shughuli zinazo tekelezwa katika kitengo hiki.