0
Your Cart
No products in the cart.

Uchumi Samawati - Rasilimali Muhimu Barani Afrika inayoweza kutimiza ndoto ya ‘Africa Tunayoitaka’

Bara Afrika ina utajiri mkubwa ki-rasilimali, kijamii na kitamaduni. Kati ya rasilimali kubwa Afrika ambayo haijatumika kikamilifu ni uchumi samawati. Kati ya nchi 54 za Afrika, 38 zina fuo ya bahari ya pwani.

 

Afrika ina takriban kilomita milioni 13 mraba za eno la bahari ikijumuisha maeneo ya kiuchumi ya bahari, takriban kilomita milioni 6.5 mraba za sakafu ya bahari, na takriban kilomita 240,000 mraba za maeneo ya ziwa. Kwa jumla, bara Afrika lina rasilimali kubwa ya bahari ambayo, ikitumiwa kikamilifu, inaweza kuchangia meandeleo endelevu kwa nchi za Afrika.

 

Matumizi endelevu, usimamizi na uhifadhi wa rasilimali na mazingira ya bahari na rasilimali zinazohusiana na rasilimali hii, ndio inafahamika kama uchumi samawati. Inajumuisha sekta nyingi kama vile uvuvi, utalii, usafiri, ujenzi wa meli, kawi, uvumbuzi wa chembechembe hai za kutengeneza dawa na bidhaa nyingine, uchimba madini chini ya bahari na shughuli husika nyinginezo.

 

Mfumo wa uchumi wa samawati unasisitiza uhusiano bora wa sekta ambazo, kwa ujumla, zinatoa huduma kutokana na kuvuna kwa viumbe hai na visivyo hai, na kufaidi nchi zenye pwani, nchi visiwa na nchi zisizo na pwani. Uchumi endelevu wa samawati pia inachangia mambo muhimu ya kijamii kama vile usawa wa jinsia, kujitosheleza kwa chakula na maji, kupunguza umaskini, uhifadhi wa utajiri, na ubunifu wa nafasi za kazi.

 

Umuhimu wa uchumi wa samawati umetambuliwa na Umoja wa Mataifa kwa kupitisha Malengo ya Maendeleo Endelevu na hasa Lengo la 14 kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zake. Umoja wa Afrika pia umetambua uchumi wa samawati kama moja ya nguzo za Agenda 2063 kuhusu Afrika Tunayoitaka.

 

Rasilimali hai zinazopatikana katika bahari ya Afrika inawezesha Afrika kuongeza uvuvi na kilimo cha maji kwa minajili ya kukuza viwanda vya dawa, kemikali na vipodozi. Ukuzaji wa viwanda kutumia rasilimali unahitaji rasilimali hai pamoja na vilengecho vingine kama vile madini na uvumbuzi wa rasilimali mpya ya kawi. Kwa hivyo, Afrika iko katikati ya biashara duniani, hasa biashara ya kuongeza ubora bidhaa.

 

Manufaa ya rasilimali hizi zitapatikana kwa urahisi na haraka ikiwa Afrika itatumia teknolojia inayofaa, ijapo Afrika iko nyuma kiteknolojia. Soko la teknolojia hai inatarajiwa kufika bilioni 5.9 za Marekani kufikia 2022. Mchango mkubwa unatazamiwa kutoka kwa uwekezaji katika utafiti wa teknolojia hai ya bahari na soko linalokuwa la viungo asili vya bahari. Teknolojia hai ni muhimu kwa kutengeneza vyakula vipya, utengenezaji madawa na vipodozi.

Mbali na viumbe hai, rasilimali ya bahari pia ina uwezo mkubwa wa kuzalisha kawi endelevu. Shirika la Kimataifa la Kawi linakisia kuwa bahari ina uwezo wa kutoa kawi endelevu mara nne ya mahitaji ya sasa ya kawi ulimwenguni. Kwa sasa, takriban asili mia 30 ya mafuta na gesi duniani inatoka baharini na inatazamiwa kuendelea kukimu mahitaji ya kawi ulimwenguni hadi pale tutakapoanza kutumia uwezo wa bahari kutoa kawi endelevu.

 

Afrika, ijapo ina rasilimali nyingi, ina athirika kutokana na janga la umaskini, ikiwa asili mia 46 ya wakazi wake wako katika umaskini mkubwa. Umoja wa Afrika umefanya bidii ya kuwahamasisha wanachama wake kuhusu umuhimu wa uchumi samawati, hasa katika kukuza utajiri na kupunguza janga la umaskini. Kwa kusisitiza umuhimu huu, Umoja wa Afrika uliunda Mkakati wa Pamoja wa Bahari, na kuweka uchumi samawati kama nguzo muhimu ya Agenda 2063 ya Afrika Tunayoitaka. Umoja wa Afrika pia ulianzisha Siku ya Mwafrika, Julai 25 na Mwongo wa Bahari (2015-2025) ili kuhamasisha mipango na kazi kuhusu uchumi samawati.

 

Kufikia sasa, nchi nyingi Afrika zimeanza kutambua umuhimu wa uchumi samawati. Baadhi ya nchi za Afrika zimeanza kuunda sera, mikakati na miongozo ya uchumi samawati kama vile Mauritius na Ushelisheli.

 

Kwa kusisitiza umuhimu huu, Umoja wa Afrika uliunda Mkakati wa Pamoja wa Bahari, na kuweka uchumi samawati kama nguzo muhimu ya Agenda 2063 ya Afrika Tunayoitaka. Umoja wa Afrika pia ulianzisha Siku ya Mwafrika, Julai 25 na Mwongo wa Bahari (2015-2025) ili kuhamasisha mipango na kazi kuhusu uchumi samawati.

 

Kufikia sasa, nchi nyingi Afrika zimeanza kutambua umuhimu wa uchumi samawati. Baadhi ya nchi za Afrika zimeanza kuunda sera, mikakati na miongozo ya uchumi samawati kama vile Mauritius na Ushelisheli.

 

Kuna changamoto ambazo zinazuia kupatikana kwa manufaa ya uchumi wa samawati. Changamoto hizi ni kama vile hatari za mabadiliko ya hali ya hewa, ukosefu wa usalama baharini, tsunami na vimbunga, ongezeko la maji baharini, ongezeko la asidi baharini, uvuvi wa kupita kiasi kutokana na uvuvi haramu na matumizi ya mbinu zisizo endelevu za uvuvi, uchafuzi na uharibifu wa maeneo ya bahari.

 

Changamoto nyingine ni kama vile ukosefu wa njia za kufikia rasilimali zinazo milikiwa kwa pamoja. Vilevile, teknolojia muafaka na uzoefu unaohitajika kufaidi uchumi samawati, imekuwa kizuizi. Malengo yasiyo sawia baina ya nchi inaweza kupunguza uwezo wa nchi kushirikiana na hata kuleta hofu kati yao.

 

Uwezo wa Afrika kunufaika na uchumi samawati utategemea pa kubwa jinsi Afrika itakavyo jifafanulia swala zima la maendeleo na ufanisi, kwa kukuza fikra bunifu. Kwa kuongezea, kuna haja ya kujumuisha vikundi vyote vya kijamii, hasa wanawake, vijana, jamii mashinani na jamii zilizo tengwa, na kutambua nafasi za kipekee ambazo wadau hawa wanaweza kuchangia ili kuleta maendeleo ya haraka.

 

Katika mchakato mzima, kuna umuhimu wa kulinda tamaduni zetu za Afrika. Maelfu ya jamii asili wanaendelea kutumia tamaduni na njia zao asili za chumo riziki. Chumo riziki hizi sio tu njia za kujipatia mapato, bali pia inawakilisha kitambulisho chao.


Bw. Moses Ziro (Mwandishi wa Makala) ni Katibu wa Watu Mazingira Ulimwenguni, na Mkurugenzi Mtendaji wa Africa Nature Organization.

Maoni Yako

Barua pepe yako haitachapishwa,

Chapisho za Hivi Karibuni

swSwahili